Graca Machel kumshtaki daktari wa Nelson Mandela
GETTY IMAGES
Mjane wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela Graca Machel, amesema atamshtaki daktari wake bwana Mandela, kutokana na taarifa alizochapisha kwenye kitabu kuhusu siku za mwisho za Mandela.
Daktari huyo Vejay Ramlakan aliongoza kikosi kilichomhudumia Mandela hadi kifo chake Disemba mwaka 2013.
Radio ya taifa nchini Musumbiji ilitangaza taarifa iliyotolewa na wakfu wa Bi Machel ikilaani kitabu hicho vikali.
- Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela yauzwa
- Winnie Mandela aibiwa dola 6000 kutoka nyumbani kwake
- Winnie Mandela aukosoa uongozi wa ANC
- Kathrada, aliyefungwa pamoja na Mandela afariki
- Jacob Zuma na makamu wake walazimishwa kusalimiana
Bi Machel alisema kuwa kitabu hicho kinakiuka heshima ya bwana Mandela.
Kitabu hicho kimeandika taarifa kuhusu siku za mwisho kabla ya kifo cha Mandela.
Kimetaja kutokuwepo kwa maelewano kati ya madaktari na familia ya Mandela.
Bi Mandela anasema kuwa kitabu hicho kilikiuka siri iliyo kati ya daktai na mgonjwa.
Leave a Comment