Mugabe ampa mkwe wake zawadi ya dola 60,000
AFP
Rais wa Zimbawe Robert Mugabe amempa mkwe wake zawadi ya dola 60,000 wakati wa siku yake ya kuzaliwa kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald.
Alisema kuwa zawadi hiyo ni ya kumshukuru Junior Gumbochuma ambaye ni dadake mkubwa wa mke wake Mugabe, Grace kwa kusaidia watoto wa Mugabe.
- Mugabe amfuta kazi mkuu wa mashtaka Zimbabwe
- Aliyetangaza ''afya ya Mugabe imedhoofika'' akamatwa
- Afya ya rais Robert Mugabe yadhoofika
Bi Gumbochumba ni mhubiri na Herald linaripoti kuwa rais alitumia fursa hiyo ya sherehe za kuzaliwa, kukosoa wahuribu wa Pentecostal ambao hupata pesa kutoka kwa waumini kwa kubuni majaabu ya uwongo.
Uchumi wa Zimbawe kwa sasa unapitia changamoto wakati nchin hiyo inakumbwa na uhaba wa pesa kutokana na uhaba wa noti za dola ambazo ndizo hutumika nchini humo.
Leave a Comment